Tuesday, May 13, 2014

FARAH KUSHIRIKI MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA.

MWANARIADHA nyota na mshindi wa medali ya olimpiki kutoka Uingereza, Mo Farah anatarajia kushindana katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika jijini Glasgow baadae mwaka huu. Farah aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwahabarisha mashabiki wake kuwa atashiriki michuano hiyo. Nyota huyo aliongeza kuwa mpaka sasa hajaamu8a kama atashindana katika mbio za mita 1,500, 5,000 au 10,000 lakini atawahabalisha pindi atakapoamua. Farah mwenye umri wa miaka 31 alishika nafasi ya nane katika mbio za Marathon za London Aprili mwaka huu na ilikuwa haijulikani kama atakuwepo katika mashindano ya Glasgow.

No comments:

Post a Comment