Tuesday, May 13, 2014

BERLUSCONI AMFUNDA BALOTELLI.

RAIS wa klabu ya AC Milan, Silvio Berlusconi anafikiri Mario Balotelli anahitaji kufanyia kazi nafasi yake na kudai kuwa mshambuliaji huyo kwasasa hajui jinsi ya kufunga mabao. Balotelli mwenye umri wa miaka 23 ndiye anaongoza kwa ufungaji mabao katika timu hiyo hiyo msimu huu akiwa amefunga mabao 14 katika mechi 19 alizocheza. Hata hivyo, Berlusconi anaamini nyota huyo wa kimataifa wa Italia anapaswa kuacha kurudi pindi anapocheza kama anataka atambulike kama mmoja wa washambuliaji hodari. Berlusconi angependa kumpa ushauri Balotelli na kama akikubali angemuambia kwamba anapaswa kukaa karibu na goli ili aweze kufunga.

No comments:

Post a Comment