Friday, May 23, 2014

BEKI WA NEWCASTLE ATISHIWA KUUAWA NA MASHABIKI WA URUGUAY.

BEKI wa klabu ya Newcastle United, Paul Dummett amepokea vitisho vya kuuawa katika mtandao kutoka kwa mashabiki wa Uruguay ambao wanamlaumu kwa majeraha ya goti aliyopata Luis Suarez. Nyota huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 27 alifanyiwa upasuaji wa goti jana lakini anategemea kupona kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwezi ujao. Mashabiki wa Uruguay walimshambulia Dummett mwenye umri wa miaka 22 kupitia mtandao wa kijamii wa twitter kwa faulo hiyo aliyomchezea Suarez katika mchezo wa Ligi Kuu baina ya timu hizo lakini haijajulikana moja kwa moja kama tukio hilo ndilo lilisababisha majeraha hao. Dimmett alitolewa nje kwa kadi nyekundu lakini baadae kadi hiyo iliondolewa. Kumekuwa hakuna ripoti yoyote ya majeraha ya Suarez katika mchezo dhidi ya Liverpool ambao walishinda mabao 2-0 lakini nyota huyo alianza kulalamika maumivu wakati akianza mazoezi na timu yake ya taifa mapema wiki hii.

No comments:

Post a Comment