Friday, May 23, 2014

PSG YAMTENGEA DAU NONO LUIZ.

BEKI mahiri wa kimataifa wa Brazil, David Luiz anakaribia kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain-PSG ndani ya saa 24 zijazo kwa dili kubwa ambalo litawagharimu matajiri hao wa Ufaransa paundi milioni 50. Makubaliano ya muda gani atakipiga huko bado hayajawekwa wazi na timu hiyo lakini uhamisho nyota huyo wa Chelsea mwenye wa miaka 27 utakuwa ni ghali zaidi kwa mchezaji wa nafasi yake ambao utawazidi Marquinos na Thiago Silva ambao wote walisajiliwa na PSG. Mara ada hiyo itakapokubaliwa na Chelsea, PSG wataomba ruhusa kutoka kwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari kusafiri kwenda katika michuano ya Kombe la Dunia kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya afya. Nchini Uingereza beki aliyewahi kununuliwa kwa kitita kikubwa alikuwa ni Rio Ferdinand wakati akiondoka Leeds kwenda Manchester United kwa ada ya paundi milioni 30.

No comments:

Post a Comment