Friday, May 23, 2014

COSTA ADAI HAOGOPI KUFUNDISHA WANAUME.

MWANAMAMA Helena Costa amedai haogopi kibarua kilichopo mbele yake baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa kocha katika timu ya soka ya wanaume. Costa mwenye umri wa miaka 36 ambaye alikuwa mng’amua vipaji wa timu Celtic amechukua mikoba ya kuinoa timu ya daraja la pili ya Clermont Foot ya Ufaransa. Akihojiwa katika mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari, Costa amesema haofii chochote kwani kama asingefikiria anaiweza kazi hiyo asingekuwa hapo. Kabla ya utauzi wa Costa, mwanamke aliyewahi kocha katika timu za wanaume barani Ulaya alikuwa Carolina Morace ambaye aliifundisha timu ya Viterbese inayoshiriki Serie C kwa mechi mbili mwaka 1999. Costa ambaye amewahi kuifundisha timu ya vijana ya wanaume ya Benfica na timu ya taifa ya wanawake ya Qatar aliteuliwa kushika wadhifa huo na rais wa Clermont Foot, Claude Michy Mei 7 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment