Friday, May 23, 2014

ROSBERG KUPEWA MKATABA MPYA MARCEDES.

DEREVA nyota wa mashindano ya langalanga Nico Rosberg anatarajiwa kubakia katika timu ya Marcedes sambamba na mwenzake Lewis Hamilton. Mkataba wa Rosberg raia wa Ujerumani unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huulakini sasa ataongeza mkataba mwingine ambao utamfanye aendelee kuwepo kwa miaka miwili zaidi. Msemaji wa Mercedes amesema katika taarifa yao kuwa timu hiyo imekuwa na mahusiano mazuri ya muda mrefu na madereva wake wote. Rosberg ambaye alishinda mashindano ya kwanza ya msimu huu wa 2014 kwasasa anashikilia nafasi pili nyuma ya Hamilton ambaye anatumikia msimu wake wa pili katika mkataba wa miaka mitatu aliosaini.

No comments:

Post a Comment