Wednesday, May 21, 2014

NYOTA WA GOFU MCLLROY AMPIGA CHINI MPENZI WAKE AMBAYE NI NYOTA WA TENISI WOZNIACKI WAKATI KADI ZA HARUSI ZIKIWA TAYARI ZIMESAMBAZWA.

MCHEZAJI nyota wa mchezo wa gofu kutoka Ireland ya Kaskazini, Rory MclIroy amevunja mahusiano yake ya uchumba na nyota wa tenisi mwanadada Caroline Wozniacki. MalIroy mwenye umri wa miaka 25 ambaye amewahi kushinda mataji mawili makubwa ya gofu na nyota huyo wa tenisi mwenye umri wa miaka 23 raia wa Denmark walitangaza kuvishana pete rasmi katika sherehe za mwaka mpya. Nyota huyo wa gofu amesema tatizo ni la kwake kwasababu baada ya kuanza kusambazwa kadi za harusi mwishoni mwa wiki iliyopita akagundua kuwa hayuko tayari kwa ajili ndoa. Wawili wamekuwa wapenzi kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.


No comments:

Post a Comment