Friday, May 2, 2014

CASILLAS ANAPASWA KUPEWA MUDA ZAIDI WA KUCHEZA - VALDANO.

MENEJA mkuu wa zamani wa Real Madrid Jorge Valdano anaamini Iker Casillas anastahili kuwa golikipa namba moja wa klabu hiyo kwa mechi za La Liga zilizobakia msimu huu ili kumuandaa kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Ligi yaMabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid. Casillas amekuwa akitumika katika michuano mingine tofauti na La Liga na kocha Carlo Ancelotti msimu huu huku Diego Lopez akianza katika mchezo wa ligi. Hata hivyo, Valdano ambaye aliondoka Santiago Bernabeu Mei mwaka 2011 anaamini kuwa muda umefika kwa golikipa huyo mwenye umri wa miaka 32 kuwa chaguo la kwanza. Valdano amesema ni kipindi kirefu mpaka kufikia fainali hivyo kama maamuzi angekuwa anafanya yeye angempa mudawa kucheza ili kumuweka fiti na kumuongezea kujiamini kabla ya mchezo huo muhimu.

No comments:

Post a Comment