Friday, May 2, 2014

PALACE, SUNDERLAND WATAWALA TUZO ZA MWEZI UINGEREZA.


MENEJA wa klabu ya Crystal Palace, Tony Pulis amepewa tuzo ya kocha bora wa mwezi Aprili wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Pulis mwenye umri wa miaka 56 aliiongoza Palace kushinda mechi nne kati ya tano walizocheza mwezi uliopita na kuifanya timu hiyo kukwea mpaka nafasi ya 11 hivyo kuepuka balaa la kushuka daraja. Kwa upande wa wachezaji, mshambuliaji nyota wa klabu ya Sunderland, Connor Wickham alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Kinda huyo mwenye miaka 21 alifunga mabao matano mwezi uliopita na kuiondosha timu yake kutoka katika mstari wa kushuka daraja huku akifunga mabao muhimu katika mechi dhidi ya Manchester City na Chelsea.

No comments:

Post a Comment