MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amesisitiza kuwa ataendelea kubakia mkweli katika mbinu zake na kudokeza kuwa yuko tayari kuacha kuifundisha kama timu hiyo itadhani sio mtu sahihi kwa kibarua hicho. Kocha huyo wa zamani wa Barcelona amekuwa akipondwa vikali kwa aina ya mchezo wake wa kumiliki mpira kwa kipindi kirefu baada ya Bayern kung’olewa katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufungwa jumla ya mabao 5-0 na Real Madrid. Pamoja na hayo,Guardiola hana mpango wowote wa kubadilisha aina ya ufundishaji ili kuwafurahisha baadhi ya wadau wa timu hiyo wanaomponda. Guardiola amesema hiyo ndio aina ya ufundishaji anayotumia na wataitumia katika mechi dhidi ya Humburg, Stuttgart na hata katika fainali ya Kombe la Ujerumani dhidi ya mahasimu wao Borussia Dortmund. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa hatakuwa ameitendea haki klabu na wachezaji wake kama hatakuwa mkweli kwao. Ni juu ya klabu kuamua kama anafaa au hafai.
No comments:
Post a Comment