Sunday, May 18, 2014

DROGBA KUIKACHA GALATASARAY.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Galatasaray, Didier Drogba ametangaza nia yake ya kuikacha timu hiyo pindi mkataba wake utakapomalizika majira ya kiangazi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 alihamia timu hiyo akitokea klabu ya Shanghai Shenhua Januari mwaka 2013 na kuisadia Galatasaray kushinda taji la Ligi Kuu la nchi hiyo sambamba na Kombe la Ligi. Akizungumza na waandishi wa habari Drogba amedai kuwa timu hiyo itabaki ndani ya moyo wake na najivunia kuwawakilisha katika kipindi chote alichokuwepo. Drogba amesema aliamua kujiunga na timu hiyo ya Uturuki siyo kwa ajili ya pesa, maana kama angehitaji pesa angebakia China lakini ikilichomomfanya kutua hapo ni msisimko wa soka.

No comments:

Post a Comment