Sunday, May 18, 2014

PIGO KATIKA KIKOSI CHA UFARANSA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps anatarajia kukosa huduma ya golikipa wa Olympique Marseille Steve Mandanda katika michuano ya Kombe la Dunia kutokana na majeruhi. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 29 alipata majeraha ya shingo katika mchezo dhidi ya Guingamp ambao Marseille walishinda kwa bao 1-0 na kulazimika kutoolewa nje katikati ya kipindi cha kwanza. Mandanda alifanyiwa vipimo zaidi leo na Marseille kutangaza kuwa golikipa huyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki zisizopungua sita. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa timu hiyo imedai kuwa Mandanda atavalishwa bandeji gumu shingoni kwa wiki tatu na atahitaji wiki tatu zingine ili aweze kupona sawasawa. Mandanda alikuwa mmoja kati ya makipa watatu walioitwa katika kikosi cha awali cha Deschamps kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika nchini Brazil sambamba na Hugo Lloris na Mickael Landreau.

No comments:

Post a Comment