Tuesday, May 6, 2014

DZEKO AJUMUISHWA KIKOSI CHA BOSNIA-HERCEGOVINA.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Edin Dzeko na golikipa wa Stoke City Asmir Bogovic ni miongoni mwa wacheza 24 walioitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Bosnia-Hercegovina kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia. Nchi iliyojitenga na iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia, na kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mwaka 1996 hiyo itakuwa mara yao ya kwanza kushiriki mashindano makubwa kama hayo. Kocha wa timu hiyo Safet Susic amesema anaamini kikosi chake kinaweza kufuzu hatua ya makundi na kuingia hatua ya mtoano katika michuano hiyo itakayofanyika nchini Brazil. Bosnia itakwaana na Argentina, Nigeria na Iran katika kundi F.

No comments:

Post a Comment