Wednesday, May 21, 2014

ETO'O AENDELEZA VITA VYAKE NA MOURINHO, AMUITA KIBARAKA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Chelsea, Samuel Eto’o ameendeleza vita vya maneno na Jose Mourinho kwa kumfananisha kocha huyo na kibaraka huku akisisitiza bado ana uwezo wa kucheza kwa kiwango cha juu. Mourinho alinaswa katika picha ya video akitoa kauli za kuponda viwango vya washambuliaji wake katika sherehe zilizoandaliwa na wadhamini huko Switzerland Februari mwaka huu na kuwadai kuwa Eto’o anaweza kuwa mkubwa kuliko anavyodai. Nyota huyo wa kimataifa wa Cameroon ambaye amefunga mabao 14 kwa msimu wake mmoja akiwa Stamford Bridge alivunja ukimya wiki iliyopita kuhusiana na suala hilo na kumumfananisha Mourinho na mpuuzi. Akiulizwa tena mahusiano yake na kocha huyo Mreno katika mahojiano na mtandao wa Cafonline Eto’o amesema ukiachana na maneno ya vibaraka kuhusiana na umri wake yeye bado yuko fiti kimwili na katika umri wa miaka 33 anajisikia vyema na ameonyesha anaweza kufanya vyema kuliko wachezaji wenye umri mdogo. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa hatakwenda Marekani au Mashariki ya Kati kwasababu bado ataendelea kucheza katika ligi zenye hadhi ya juu kwasababu mapenzi yake na michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bado hayajaisha.

No comments:

Post a Comment