Tuesday, May 6, 2014

FEDERER AJITOA MICHUANO YA MADRID MASTERS ILI KUMHUDUMIA MKEWE.

MCHEZAJI tenisi nyota anayeshika namba nne katika orodha za ubora duniani, Roger Federer amejitoa katika michuano ya Madrid Masters iliyoanza wiki hii ili aweze kuwa karibu na mke wake Mirka ambaye anakaribia kujifungua mtoto wao wa tatu. Federer alisema katika michuano ya Monte Carlo Masters mwezi uliopita kuwa hata kuwa na kinyongo chochote kwa kukosa michuano yoyote hata ya wazi ya Ufaransa ili aweze kuwa na mkewe katika siku hiyo muhimu. Nyota huyo aliwaomba radhi mashabiki wake na ana matumaini ya kurejea tena Madrid mwaka ujao. Michuano ya Rome Masters na French Open pia inatarajiwa kuchezwa mwezi huu wa Mei.

No comments:

Post a Comment