MENEJA wa muda wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs aliandaa shughuli maalumu huko Carrington jana wakati klabu hiyo ikiwa katika maandalizi ya kumtangaza Louis van Gaal kama kocha mpya wa kudumu. Kumekuwa na tetesi zilizozagaa toka April mwaka huu kuwa Van Gaal tayari amekubali dili la kutua Old Trafford baada ya kumaliza majukumu yake katika timu ya taifa ya Uholanzi baada ya Kombe la Dunia. Wakati msimu ukielekea mwishoni Giggs alikialika kikosi kizima, viongozi, wafanyakazi na wapendwa wao katika uwanja huo wa mazoezi kwa kile kilichoonekana kama kuagana nao baada ya kukaa nao kwa miongo kadhaa. Giggs na wachezaji wenzake wa darasa la mwaka 1992 akiwemo Nick Butt, Phil Neville na Paul Scholes hawana uhakika na mustakabali wao huko mbele pindi atakapokuja Van Gaal ambaye anatarajiwa kuitangazwa siku zisizozidi 10.
No comments:
Post a Comment