MENEJA wa muda wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs amechukizwa na kiwango kibovu cha timu yake katika mechi za nyumbani baada ya kupokea kipigo kutoka Sunderland jana. Bao pekee la Sebastian Larsson lilitosha kuifanya United kuchwapwa mara saba katika Uwanja wa Old Trafford, ikiwa ni kiwango kibovu toka walipofanya hivyo msimu wa 1973-1974 wakati waliposhuka daraja. Giggs ambaye huo ulikuwa mchezo wake wa pili toka achukue mikoba ya muda kutoka David Moyes aliyetimuliwa amesema hajui kwanini kiwango chao katika mechi nyumbani kimekuwa sio cha kuridhisha kabisa msimu huu. Wakiwa wamebakiwa na michezo miwili United waliopo nafasi ya saba hawawezi tena kukwea juu kuzidi nafasi ya sita baada ya ushindi huo wa kwanza wa ligi kwa Sunderland katika Uwanja wa Old Trafford toka mwaka 1968.
No comments:
Post a Comment