Sunday, May 4, 2014

GAMBIA YAFUNGIWA MIAKA MIWILI NA CAF KWA KUDANGANYA UMRI.

KAMATI ya utendaji ya Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF limekisimamisha Chama cha Soka nchini Gambia kushiriki mashindano yoyote ya shirikisho hilo kwa miaka miwili baada kudanganya umri wa wachezaji. Mwezi uliopita Gambia walienguliwa katika mechi za kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 kwa kuchezesha wachezaji waliozidi umri. Sasa, nchi hiyo imefungiwa kushiriki michuano yoyote inayoandaliwa na CAf ikiwemo michuano ya Mataifa ya Afrika 2015 kwa kukiuka sheria hiyo. Kufungiwa kwa Gambia kunamaanisha kuwa Shelisheli itakuwa imesonga mbele katika mzunguko wa pili ya kufuzu michuano hiyo mwakani. Mbali na kufungiwa timu ya taifa, vilabu vya Gambia navyo havitaruhusiwa kushiriki mashindano ya vilabu yanayoandaliwa na CAF kwa kiindi kama hicho cha miaka miwili.

No comments:

Post a Comment