NGULI wa soka wa klabu ya Arsenal, Tony Adams amekutaka na rais wa Rwanda ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa timu hiyo Paul Kagame jijini Kigali jana. Wawili hao walikutana ikulu ambapo walifanya mazungumzo ya mambo mbalimbali kuhusiana na klabu hiyo wanayoipenda. Adams ambaye alifika Kigali toka Alhamisi amesema amefurahi kukutana na kiongozi huyo kwani ni mshabiki wa kweli wa Arsenal na walizungumza mengi kuhusiana na timu hiyo. Mbali na kuzungumzia hayo, Adams pia alimfahamisha kiongozi huyo sababu ya ziara yake ambayo ni kukuza hadhi ya mchezo wa soka katika eneo hilo kupitia kliniki ya mafunzo ambayo imewezeshwa na mpango wa Airtel Rising Stars wenye ubia na Arsenal.
No comments:
Post a Comment