BEKI wa Bayern Munich, Jerome Boateng anatarajiwa kulimwa faini na klabu yake kwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo walioshindamabao 4-1 dhidi ya Hamburg SV jana baada ya kumnasa kofi mchezaji wa upinzani. Ofisa Mkuu wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge amesema kitendo kilichofanywa na nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani dhidi ya Kemel Demirbay wa Hamburg katika dakika ya 86 ni utovu wa nidhamu wa wazi. Rumminigge amesema tukio alilofanya Boateng halikuwa la lazima ndio maana wameamua kumchukulia hatua ili kulinda nidhamu katika timu. Beki huyo ambaye alianza kwa kumgusa kwa kichwa Demirbay na baadae kumnasa kofi anatarajiwa kutajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani wiki ijayo kwa ajili ya Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment