SHABIKI wa soka wa Brazil amefariki dunia baada ya kupigwa na sinki la chooni lililorishwa mwishoni mwa mchezo wa Ligi Daraja la Pili huko Recife mji uliopo kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo. Shabiki huyo Paulo Ricardo Gomes da Silva alipatwa na mswahibu hayo wakati vurugu zilipozuka karibu na moja ya milango ya kuingilia Uwanja wa Arruda. Watu wengine watatu wanaroptiwa kuumia wakati masinki hayo ya chooni yalipokuwa yaking’olewa kutoka mahali yalipowekwa na kurushiwa mashabiki wapinzani waliokuwa wamekaa upande wa chini wa jukwaa. Recife ni mji mojawapo utakaotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia linatarajiwa kuanza Juni 12 mwaka huu lakini mechi zake zitacheza katika uwanja mwingine wa Arena Pernambuco ambao umejengwa mahsusi kwajili ya michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment