MENEJA wa klabu ya Barcelona, Gerardo Martino amedai kuwa hastahili kupewa msimu mwingine kuifundisha timu hiyo baada ya sare ya mabao 2-2 waliyopata dhidi ya Getafe jana hivyo kufifisha matumaini yao ya kutetea taji la La Liga. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Martino amesema huo sio mwisho alioutarajia na kwa mawazo yake haukuwa msimu mzuri kwake na hata kwa Barcelona kwasababu sivyo walivyozoea. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa msimu ulikuwa mgumu huku kukiwa na matatizo mengi nje ya uwanja na walijaribu kadri walivyoweza kusahau matatizo hayo kwa kucheza hatua mbayo haijawafikisha pabaya mpaka leo. Martino amesema pamoja na matatizo yote hayo waliyopitia bado anadhani lawama zote zinapaswa kumuangukia yeye kwasababu ameshindwa kuifikisha timu mahali walipozoea.
No comments:
Post a Comment