Friday, May 23, 2014

MADRID WATUA LISBON TAYARI KUIKABILI ATLETICO KATIKA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amevuta hisia kubwa wakati aliporejea tena jijini Lisbon jana jioni wakati timu hiyo ilipotua nchini Ureno kuelekea katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alionekana kuwa mtulivu huku akizungumza na mchezaji mwenzake Pepe baada ya kushuka kutoka katika ndege binafsi ya timu hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Lisbon, ikiwa yamebaki masaa machache kabla ya mchezo huo utakaofanyika huko Estadio da Luz. 
Ronaldo amerejea tena katika mji huo mkuu ambako alikaa miaka sita akiichezea timu ya Sporting Lisbon kabla ya kwenda Manchester United mwaka 2003 huku akiwa na uhakika wa kuwepo katika kikosi cha kwanza cha Carlo Ancelotti katika mchezo huo dhidi ya Atletico. Nyota huyo Mreno hajakuwepo katika kikosi cha Madrid toka walipotoa sare ya bao 1-1 na Villadolid Mei 7 mwaka huu ambapo alitolewa dakika nane ya mchezo kwasababu ya kuumia. Pamoja na hofu juu ya afya ya mchezaji huo, Ancelotti aliwaondoa hofu hiyo mashabiki wa Madrid kwa kuthibitisha kuwa Ronaldo ayakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kesho.

No comments:

Post a Comment