Friday, May 23, 2014

PSG YAENDELEZA KUFURU ZA KUTUMIA FEDHA KWA KUMSAJILI LUIZ KWA DAU LA KUVUNJA REKODI.

KLABU ya Chelsea imefikia makubaliano na timu ya Paris Saint-Germain-PSG ya mauzo ya kiasi cha paundi milioni 40 kwa ajili ya beki wake David Luiz. Luiz mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Chelsea kwa ada ya paundi milioni 21.3 akitokea klabu ya Benfica ya Ureno Januari mwaka 2011. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa Chelsea imedai kuwa uhamisho huo umekubaliwa pia na mchezaji mwenyewe kuhusiana na mahitaji yake binafsi na tayari amefaulu vipimo vya afya. Beki huyo wa kimataifa wa Brazil alikuwa amebakisha mkataba wa miaka mitatu kati ya mitano aliyosaini Stamford Bridge Septemba mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment