Sunday, May 18, 2014

MANGALA AITAMANI CHELSEA.

BEKI wa klabu ya Porto, Eliaquim Mangala amesema kuwa angependa kujiunga na Chelsea kuliko mabingwa wa Ligi Kuu Manchester City wakati joto la usajili kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 likiwa juu katika majira haya ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa na msimu mzuri nchini Ureno hatua ambayo imeibua tetesi za kuhamia katika vilabu vikubwa ikiwemo City katika majira ya usajili Januari ingawa walishindwa kuafikiana bei. Lakini hata kama City wakiamua kumfukuzia nyota huyo majira haya ya kiangazi, beki huyo wa kati amesema angefurahi zaidi kwenda Chelsea na kuonya kuwa usajili wowote itabidi usubiri baada ya michuano ya Kombe la Dunia. Mangala amesema pamoja na kutoa msimamo wake huo lakini fikra na mawazo yake kwasasa yameelekea Brazil kwa ajili ya michuano hiyo na baada ya hapo ndipo atakapofikiria mustakali wake.

No comments:

Post a Comment