Sunday, May 18, 2014

UZI WA MWISHO WA ARSENAL KUHITIMISHA MIAKA 20 YA MKATABA NA KAMPUNI YA NIKE.

KLABU ya Arsenal imetoa jezi mpya baada ya kutwaa Kombe la FA kusherehekea miaka 20 ya uhusiano wao na Nike ambao umefikia tamati mwishoni mwa msimu huu. Ni jezi yenye mwonekano tofauti na jezi za miaka mingi iliyopita Arsenal na zinakuja baada ya kumaliza ukame wa miaka tisa wa mataji. Arsenal walitwaa Kombe la FA Jumamosi baada ya kuifunga Hull City 3-2 katika Uwanja wa Wembley.

No comments:

Post a Comment