Thursday, May 29, 2014

MINALA AJISAFISHA BAADA YA KUGUNDULIKA KUWA HAKUDANGANYA UMRI WAKE.

CHAMA cha Soka nchini Italia kimethibitisha kuwa kiungo wa klabu ya Lazio, Joseph Minala hakudanganya kuhusiana na umri wake. Mtandao mmoja wa soka barani Afrika ulitoa madai Februari mwaka huu kuwa Minala ambaye ni mzaliwa wa Cameroon ana umri wa miaka 42 na sio miaka 17 anayotaja yeye. Suala hilo lilipelekea maofisa kufanyia uchunguzi taarifa hizo ambapo ilipelekea Manala mwenye kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo. Katika taarifa yake mara baada ya uchunguzi FIGC ilidai kuwa hawakupata ushahidi wowote ambao ungepelekea hatua za nidhamu kuchukuliwa. Minala alijiunga na Lazio yenye maskani yake jijini Rome majira ya kiangazi mwaka jana na aliiwakilisha timu hiyo katika michuano ya vijana ya Kombe la Viareggio Februari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment