Thursday, May 29, 2014

ARSENAL WAMPANDIA NDEGE MORATA.

MAOFISA wa klabu ya Arsenal, wamesafiri kwenda Hispania kwa matumaini ya kumamilisha dili kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata. Mshambuliaji huyo amekuwa akiwindwa na Arsene Wenger kwa muda mrefu na klabu imeamua kuanza harakati za kumsajili nyota huyo mwenye miaka 21 mapema, kwani Juventus nao pia wanamuwinda. Madrid wako tayari kumuuza lakini wanatarajiwa kusisitiza kutaka dau lao walilomnunulia kitu ambacho kinaonekana kitakuwa kigingi kikubwa kwa timu zinazomuhitaji. Arsenal walijaribu kumsajili kinda huyo wa kimataifa wa Hispania majra ya kiangazi mwaka jana na safari hii wanaamini uhakika wa kupata namba katika kikosi cha kwanza atakaoupata utawasaidia kumvutia kwao. Morata amefunga mabao tisa katika mechi 28 alizocheza akiwa na Madrid msimu huu na alitokea benchi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika Jumamosi na kuisadia timu yake kuisambaratisha Atletico Madrid. Arsenal pia wanamtaka mshambuliaji mwingine wa Madrid Karim Benzema lakini Carlo Ancelotti anamtaka nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kusaini mkataba mpya na timu hiyo.

No comments:

Post a Comment