Thursday, May 29, 2014

MAJERUHI YAMKOSESHA WOODS MICHUANO YA US OPEN.

MCHEZAJI nyota wa gofu, Tiger Woods amejitoa katika michuano ijayo ya wazi ya Marekani ili aweze kupona sawasawa kufuatia upasuaji wa mgongo aliofanyiwa. Woods mwenye umri wa miaka 38 raia wa Marekani ambaye ni bingwa wa mataji makubwa 14 ya gofu, hajaonekana katika viwnaja vya gofu toka alipocheza michuano ya WGC-Cadillac Machi mwaka huu. Nyota huyo ambaye kwasasa ameporomoka katika orodha za ubora duniani mpaka nafasi ya tatu alikaririwa katika mtandao wake akidai kuwa bado hayuko fiti kwa ajili ya mashindano. Taarifa yake iliendelea kudai kuwa pamoja na kukosa mashindano mawili makubwa ya mwanzo na michuano mingine muhimu bado anaamini atarejea tena uwanjani mwaka huu. Woods alikosa michuano ya Masters iliyofanyika April mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza toka aanze kucheza mchezo huo baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.

No comments:

Post a Comment