Thursday, May 29, 2014

HATUNA MATATIZO YA KIFEDHA YATAKAYOTULAZIMU KUUZA NYOTA WETU - MARIN.

OFISA mkuu wa klabu ya Atletico Madrid Angel Gil Marin amezionya timu zote barani Ulaya kuwa hawahitaji kuuza mchezaji yoyote kwa ajili ya matatizo ya kifedha. Baadhi ya wachezaji muhimu wa timu hiyo wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kuondoka Vicente Calderon baada ya msimu mzuri ambao uliwasaidia kushinda taji la La Liga na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Pamoja na kuwa na nguvu ndogo za kiuchumi kulinganisha na wapinzani wao Real Madrid na Barcelona, Marin amesema hawana haja ya kuuza wachezaji wao ili waweze kuinuka kiuchumi. Marin pia alidokeza kuwa kunaweza kuwa na mikataba mipya na iliyoboreshwa kwa baadhi ya wachezaji wao huku nyota waliong’ara msimu huu kama Diego Costa, Miranda na Raul Garcia wakiripotiwa kuwindwa na vilabu vikubwa barani humo. Katika taarifa yake iliyotumwa katika mtandao wa timu hiyo Marin amesema hawana haja ya kuuza mchezaji yoyote katika kikosi chao cha kwanza ili waweze kuweka mahesabu yao sawa kwani wako tayari kuwaboreshea mikataba yao na kuwapa minono zaidi.

No comments:

Post a Comment