Thursday, May 29, 2014

FABIANSKI AKUBALI KWENDA SWANSEA.

GOLIKIPA wa Arsenal, Lukasz Fabianski amekubali kujiunga na Swansea City wakati mkataba wake na klabu hiyo utakapomalizika mwezi ujao. Golikipa huyo wa kimataifa wa Poland alikataa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ili kumzuia asiondoke na sasa ameamua kuhamia katika Uwanja wa Liberty unatumiwa na Swansea. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao, Arsenal walithibitisha kuondoka kwake na kumshukuru golikipa huyo kwa mchango wake aliotoa katika kipindi chote alichokuwepo na kumtakia kila la kheri huko anapokwenda. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Arsenal akitokea Legia Warsaw mwaka 2007 na kucheza mechi 78 katika kikosi cha kwanza katika mashidano toka alipojiunga nao.

No comments:

Post a Comment