Thursday, May 29, 2014

BARCELONA BADO VIWANGO - XAVI.

KIUNGO mahiri wa Barcelona, Xavi amesisitiza kuwa klabu hiyo bado itabakia kama moja ya timu kubwa duniani na anafikiri timu bora pekee ndio zinaweza kuifunga. Barcelona walipoteza taji la La Liga kwa Atletico Madrid huku waking’olewa na vijana haohao wa Diego Simeone katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Real Madrid wakiwatambia kwa kuwafunga katika fainali ya Kombe la Mfalme. Pamoja na hayo Xavi haamini kama msimu uliopita unatoa ishara kwamba zama zao za kutamba zimekwisha. Xavi amesema wamekosa taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufungwa na timu hiyohiyo Atletico ambao walishinda taji la ligi na kuwa washindi wa pili Ulaya ndio maana anasema timu bora pekee ndio itakayoweza kuifunga Barcelona. Mara ya mwisho Barcelona kumaliza msimu mikono mitupu yaani bila taji lolote ilikuwa msimu wa mwaka 2007-2008.

No comments:

Post a Comment