Thursday, May 29, 2014

WENGER ALIIPA TIMU YA TAIFA KIPAUMBELE KULIKO KLABU - WILSHERE.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger alikataa kumuharakisha kumchezesha Jack Wilshere baada ya kuumia kwasababu alikuwa akitaka kuhakikisha kiungo huyo anakuwa fiti kwa ajili ya Kombe la Dunia. Wilshere amesema Wenger ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa soka la kimataifa katika siku za nyuma alijiandaa kujitoa muhanga kwa balaa la majeruhi la muda lililoikumba Arsenal mwishoni mwa msimu ili aweze kuisadia timu ya taifa. Wilshere ambaye aliumia mguu akiwa katika majukumu ya kimataifa katika mechi kati ya Uingereza na Denmark Machi mwaka huu amesema alikuwa akidhani yuko tayari lakini Wenger alimkatalia kwa kumtaka afanye mazoezi zaidi ili awe fiti kwa ajili ya Kombe la Dunia. Nyota huyo mwenye miaka 22 amesema alijisikia furaha kupata ushauri huo mzuri kutoka kwa meneja wake ambaye ana uzoefu wa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment