Thursday, May 29, 2014

OSCAR AKANUSHA TETESI ZA KUTEMWA BRAZIL.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Brazil, Oscar amesema ameruhusiwa kuondoka katika kambi ya maandalizi ya nchi yake kwa ajili ya Kombe la Dunia ili aweze kuwepo hospitali wakati mtoto wake atapozaliwa katika siku chache zijazo. Kiungo huyo wa Chelsea aliandika katika mtandao wa kijamii kuwa bado yupo na mtoto wake bado hajazaliwa hivyo kuondoa uvumi uliozagaa kuwa anaweza kuwa ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa kutokana na majeruhi. Oscar aliendelea kueleza kuwa bado anasubiri na hajaondoka katika kikosi cha nchi hiyo na kwa uwezo wa mungu mtoto wake atazaliwa salama. Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kilianza mazoezi yake jana ikiwa ni siku mbili toka wakutane katika kambi yao ya Granja Comary iliyopo nje kidogo ya jiji la Rio de Janeiro.

No comments:

Post a Comment