Wednesday, May 21, 2014

PIQUE KUSAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MINNE.

BEKI wa klabu ya Barcelona Gerard Pique amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka minne na timu hiyo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 anatarajiwa kusaini mkataba huo ambao utamuweka Camp Nou mpaka 2019 katika siku chache zijazo. Pique ambaye aliwahi kuichezea Manchester United kati ya mwaka 2004 na 2008, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika Juni 2015. Toka aliporejea Barcelona ambapo alianza katika timu ya watoto, Pique amecheza mechi 266, kushinda mataji manne ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Habari hizo za kukaribia kusaini mkataba mpya zimekuja ikiwa imepita siku moja baada ya klabu hiyo kutangaza Lionel Messi kusaini mkataba mpya na mchezaji wa zamani Luis Enrique kuwa kocha mpya wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment