Wednesday, May 21, 2014

CESAR KUREJEA QPR.

GOLIKIPA Julio Cesar anayecheza kwa mkopo katika timu ya Toronto ya nchini Marekani amedai kuwa klabu yake ya Queens Park Rangers-QPR inamuhitaji kurudi baada ya michuano ya Kombe la Dunia. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil alikutanishwa na beki wa zamani wa QPR na sasa kocha wa Toronto, Ryan Nelsen Februari ili kujiunga na timu hiyo kwa mkataba wa muda wakati timu hiyo iliposhuka daraja. Mkataba wa Cesar bado unamuhitaji kubakia Marekani mpaka Desemba mwaka huu lakini inaonekana atarejea tena Uingereza kwa ajili ya msimu mpya huku QPR wakibakisha kushinda mchezo mmoja wa mtoano dhidi ya Derby County kwa ajili ya kurejea katika Ligi Kuu msimu ujao. Cesar alifafanua kuwa itategemea itakavyokuwa baada ya Kombe la Dunia lakini QPR wamesema wanamhitaji Agosti kwa ajili ya msimu mpya ligi.

No comments:

Post a Comment