Monday, May 12, 2014

PISTOROUS ANASUMBULIWA NA MARADHI YA UOGA - SHAHIDI.

MTAALAMU wa saikologia amesema kuwa mwanariadha nyota mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya woga toka akiwa mdogo na alikuwa mwoga wa mambo ya uhalifu. Mtaalamu huyo Meryl Vorster aliyekuwa akitoa ushahidi wake katika kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha huyo, amesema tukio la Pistorius kumfyatulia risasi na kumuua mpenzi wake mwaka jana linatakiwa kuchukuliwa kama ni uoga. Mwanariadha huyo amekanusha kumuua mpenzi wake Reeva Steekamp kwa makusudi akidai kuwa alidhani alikuwa amevamiwa na majambazi nyumbani kwake. Pande zote mbili za utetezi na mashitaka zinategemewa kuwa zimekamiliza ushahidi wao mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment