KIUNGO wa klabu ya Borussia Dortmund, Marco Reus amesisitiza kuwa hana mpango wa kuhama timu hiyo katika majira ya kiangazi pamoja na tetesi zilizomhusisha na kuhamia Manchester United. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu na United wameonyesha ya kumsajili ili kuongeza nguvu katika kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao. Hata hivyo, Reus amekanusha tetesi hizo na kudai kuwa bado anataka kubakia Dortmund walau kwa msimu mmoja zaidi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye ana mkataba na Dortmund mpaka 2017 amefunga mabao 23 katika mechi 43 alizocheza msimu huu katika mashindano yote.
No comments:
Post a Comment