MMILIKI wa klabu ya Aston Villa, Randy Lerner ametangaza kuiweka sokoni kwa ajili ya kuiuza timu hiyo. Mmarekani huyo aliinunua timu hiyo mwaka 2006 baada ya hisa zake za paundi milioni 62.6 kukubalika na bodi ya klabu hiyo. Katika taarifa yake Lerner amesema anataka klabu hiyo iendelee kuanza upya na kubadilisha uongozi baada ya kuona hawezi kufanya kazi hiyo. Villa imemaliza msimu wa Ligi Kuu ikiwa katika nafasi ya 15, ikiwa imeponea kushuka daraja kwa tofauti ya alama tano pekee..
No comments:
Post a Comment