MCHEZAJI nyota wa Schalke, Julian Draxler ameweka wazi kuwa ameamua kubakia katika klabu hiyo kwa msimu mmoja zaidi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani alibakia kidigo ajiunge na Arsenal katika kipindi cha dirisha dogo Januari lakini uhamisho wake ulishindikana baada ya pande zote mbili kushindwa kufikia makubaliano. Draxler bado anabakia kama mmoja wa wachezaji chipukizi anayeiwindwa na vilabu vingi barani Ulaya lakini mwenyewe amedai mustakabali wake bado unabakia katika timu hiyo hiyo. Akihojiwa Draxler amesema hana nia wala mawazo yoyote ya kuondoka Schalke kwasasa kwasababu bado anapenda kuitumikia timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment