Saturday, May 24, 2014

ROAD TO BRAZIL: RONALDINHO AAMUA KUPIGA HELA KIVINGINE KWA KULIPANGISHA JUMBA LAKE LA KIFAHARI.

BAADA ya kutemwa katika kikosi cha timu ya ya Brazil na kocha Luiz Felipe Scolari kwa ajili ya Kombe la Dunia, Ronaldinho amekuja na mbinu nyingine ya kumfanya kujipatia kipato katika michuano hiyo ya mwaka huu. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona ameamua kukodisha jumba lake la kifahari lililopo jijini Rio de Janeiro kwa paundi 9,120 kwa usiku mmoja ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuishi katika jumba lake. Ronaldo alithibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwa jumba lake hilo lenye vyumba vitano linakodishwa kupitia kampuni ya Airbnb.com wakati michuano hiyo itakayofanyika kiangazi hiki. 
Jumba hilo ambalo linajumisha mabafu sita liko eneo maalamu lenye ulinzi mkali la Barra da Tijuca. Ronaldinho amelipamba jumba lake hilo kw apicha zake wakati akicheza katika timu za Paris Saint-Germain, AC Milan na timu yake ya taifa ya Brazil. Mtu anayetaka kupanga anatakiwa kutoa malipo ya awali ya paundi 600, lakini hairuhusiwi kuvuta sigara ndani, labda nje ya nyumba na kutakuwa na timu maalum ya watu wa kuhudumia wageni.

No comments:

Post a Comment