Saturday, May 24, 2014

YAYA TOURE HATIHATI KOMBE LA DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka la Ivory Coast limethibitisha kuwa Yaya Toure anapatiwa matibabu nchini Qatar kwa majeraha ambayo hayajawekwa wazi kabla ya kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya kambi yao ya mazoezi ya Kombe la Dunia iliyopo Marekani. Toure ni mchezaji pekee kati ya 28 walioteuliwa katika kikosi cha awali cha kocha Sabri Lamouchi kukosa mwanzo wa maandalizi ya Kombe la Dunia katika kambi yao iliyopo jijini Dallas. Katika taarifa ya shirikisho hilo imedai kuwa Toure atasafiri kuelekea Marekani Alhamisi ijayo. Hospitali ya moja inayojihusisha na matibabu ya michezo iliyopo jijini Doha ilithibitisha kumpokea mchezaji huyo kwa kile walichokiita katika taarifa yao majeraha madogo. Ivory Coast inatarajia kucheza mechi zake za kujipima nguvu nchini humo dhidi ya Bosnia mchezo utakaofanyika Mei 30 huko St Louis na El Salvador utakaofanyika huko Dallas Juni 4 kabla ya kuelekea Brazil Juni 6 mwaka huu. Ivory Coast wamepangwa kundi C sambamba na timu za Colombia, Ugiriki na Japan katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 12.

No comments:

Post a Comment