Saturday, May 24, 2014

ROBBEN AITOLEA NJE MANCHESTER UNITED.

WINGA mahiri wa klabu ya Bayern Munich Arjen Robben ameitolea nje Manchester United na kusisitiza kuwa hana sababu yoyote yakumfanya aondoke Alleanz Arena kiangazi hiki. Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford ambapo angeungana na kocha wake wa zamani Louis van Gaal. Robben mwenye umri wa miaka 30 amesema angekuwa tayari kurejea nchini Uingereza kama angekuwa hana furaha mahali alipo lakini anafurahia maisha yake jijini Munich. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa United sio chaguo lake kwasasa kwani bado anapenda kubakia Bayern na hadhani kama timu hiyo itamuuza kwasababu ndio kwanza ameongeza mkataba mpya. Mbali na kukataa kujiunga na United Robben alisifu uteuzi wa Van Gaal na kudai kuwa utaisadia timu hiyo kurejesha hadhi yake.

No comments:

Post a Comment