Saturday, May 24, 2014

MANCINI AMPIGIA DEBE DROGBA KWENDA JUVENTUS.

MENEJA wa klabu ya Galatasaray, Roberto Mancini ameishauri Juventus kumsajili Didier Drogba ambaye anaondoka kwa wakongwe hao wa jiji la Instabul kiangazi hiki. Mkongwe huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia jijini Turin baada ya kuisaidia Galatasaray kushinda taji la Ligi Kuu pamoja na Kombe la Ligi katika miezi minane ambayo amekuwa nchini Uturuki. Mancini anaamini kuwa Juventus watafanya vyema kumsajili Drogba wakati wakijipanga kutetea taji lao la Serie A sambamba kampeni zao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Akihojiwa Mancini amesema kama Juventus wakimchukua Drogba watakuwa wamefanya usajili mzuri kwani nyota huyo bado anaweza kuwasaidia na kupata matokeo wanayotaka katika mashindano yote.

No comments:

Post a Comment