Saturday, May 24, 2014

ROAD TO BRAZIL: KLINSMANN AJITETEA KUMUACHA DONOVAN KATIKA KIKOSI CHAKE INGAWA AMEKIRI ULIKUWA UAUZI MGUMU.

KOCHA wa timu ya taifa ya Marekani, Jurgen Klinsmann ametetea uamuzi wake wa kumuacha Landon Donovan katika kikosi cha wachezaji 23 watakaocheza Kombe la Dunia lakini amekiri ulikuwa ni mmoja ya uamuzi mgumu kuwahi kufanya akiwa kama kocha. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 alitangaza Alhamisi kuwa Donovan hatakuwa katika mipango yake kwa ajili ya michuano hiyo pamoja na kucheza mechi 156 na kufunga mabao 57 kwa nchi yake. Kuachwa kwa Donovan kulizua mshituko mkubwa haswa ikizingatiwa kila mtu alitegemea kiungo huyo mkongwe kuwemo katika kikosi hicho ambapo zingekuwa fainali zake za nne kushiriki. Klinsmann amesema ulikuwa uamuzi mgumu kwani alikuwa na mshambuliaji mwingine ambaye anamzidi Donovan kwa maeneo kadhaa. Kocha huyo Mjerumani aliendelea kudai kuwa ilikuwa vigumu kutoa habari hivyo lakini anashukuru kwani Donovan mwenyewe amechukulia vyema uamuzi wake.

No comments:

Post a Comment