Tuesday, May 27, 2014

SUAREZ BADO MGUU NJE MGUU NDANI KOMBE LA DUNIA.

DAKTARI Alberto Pan aliyemfanyia upasuaji wa goti mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez amekataa kutoa muda rasmi wa mchezaji huyo kurejea uwanjani. Uwepo wa Suarez katika kikosi cha Uruguay kitakachoshiriki Kombe la Dunia umekuwa mashakani baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti wiki iliyopita. Pan amesema nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 anaendelea vyema na bado anaweza kusafiri kwenda Brazil lakini hana uhakika juu ya wakati ambao atakuwa fiti kwa ajili ya kucheza. Daktari huyo aliendelea kudai kuwa ni jambo la hatari kutoa muda wa mchezaji huyo kuweza kucheza kwani itategemea na jinsi anatakavyopona, kitu cha msingi anachoweza kusema ni kwamba matumaini ya kwenda Brazil bado yapo.

No comments:

Post a Comment