Tuesday, May 27, 2014

RODGERS AONGEZEWA MKATABA LIVERPOOL.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amesaini mkataba mpya wa muda mrefu na timu hiyo. Rodgers ambaye aliteuliwa kuchukua nafasi ya Kenny Dalglish mwaka 2012 aliiongoza timu hiyo kurejea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kufuatia kukosekana kwa miaka mine. Mara baada ya kusaini mkataba huo Rodgers mwenye umri wa miaka 41 amesema ni heshima kubwa kwake kupata nafasi hiyo katika klabu hiyo kubwa. Liverpool walimaliza katika nafasi ya pili wakitofautiana kwa alama mbili na mabingwa wa Ligi Kuu Manchester City.

No comments:

Post a Comment