Tuesday, May 27, 2014

ROAD TO BRAZIL: HOTELI ZITAKAZOFIKIWA NA UINGEREZA NA ITALIA ZAKUTWA NA DOSARI YA VYAKULA VILIVYOPITILIZA MUDA.

MAOFISA wa afya na usalama nchini Brazil wamevamia hoteli ambazo zitafikiwa na timu za taifa za Uingereza na Italia kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwezi ujao na kuwanyang’anya samaki, jibini na vyakula vingine ambavyo muda wake wa kuuzwa umepitiliza. Zaidi ya kilo 50 za chakula zilizogundulika hazifai kwa matumizi zilichukuliwa katika hoteli ya Portobello ambapo timu ya Italia itafikia na kilo zingine mbili ziliondolewa katika hoteli watakayofikia Uingereza ya Royal Tulip, hoteli zote hizo ziko nje kidogo ya jiji la Rio de Janeiro. Ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Kamati Maalumu ya Ulinzi na Utetezi kwa Wateja, maofisa walitembelea migahawa 13, maduka makubwa, sehemu za kuchomea mikate, maduka na hoteli na kugundua nane kati ya hizo zimekiuka taratibu. Katika taarifa yake kamati hiyo imesema jumla ya kilo 218 za chakula kisichofaa kwa matumizi kilichogunduliwa kilitupwa. Maofisa hao pia walitembelea hoteli ya Caesar Park ambayo itafikiwa na timu ya taifa ya Uholanzi lakini hawakukuta tatizo lolote. Timu 32 ambazo zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ya ikiwa ni ya kwanza kufanyika nchini humo toka ile ya mwaka 1950, nyingi kati hizo zitawenda na chakula chao pamoja na wapishi

No comments:

Post a Comment