Tuesday, May 27, 2014

SITISHIKI NA TETESI ZOZOTE ZA USAJILI JUU YANGU - LALLANA.

KIUNGO wa klabu ya Southampton Adam Lallana amesema hawezi kusumbuliwa na tetesi juu ya mustakabali wake wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa na timu ya taifa ya Uingereza. Nyota mwenye umri wa miaka 26 ametajwa kutengewa dau na Liverpool wakati akiwa katika maandalizi ya michuano ya Kombe la dunia ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 12 mwaka huu. Lallan amesema kama mustakabali utaamuliwa kabla au baada ya Kombe la Dunia hautakuwa na tofauti yoyote kwake kwani hivi sasa anatilia mkazo michuano hiyo iliyo mbele yake na kuhakikisha anacheza vyema kadri anavyoweza. Lallan ambaye alijiunga na Southampton mwaka 200, amefunga mabao 10 katika mechi 42 alizocheza msimu huu na kuisadia timu yake kumaliza katika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu nafasi ambayo ni ya juu zaidi kufikiwa toka wapande daraja. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa miaka minne iliyopita alikuwa akicheza Ligi Daraja Kwanza na alikuwa alikuwa akitizama Kombe la Dunia akiwa na wachezaji wenzake na kama mtu angemuambia kuwa atashiriki michuano itakayofuata asingeweza kumuamini kwa kipindi kile.

No comments:

Post a Comment