MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa hana mpango wa kuwaachia kuondoka wachezaji wake nyota katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Wachezaji kadhaa wa Arsenal wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kuondoka katika kipindi cha karibuni huku Bacary Sagna akiwa bado hajakubali kusaini mkataba mpya lakini Wenger amepania kukiweka kikosi chake pamoja. Akihojiwa Wenger amesema anataka wachezaji wake wote kubakia kwasababu timu hiyo ina malengo makubwa huko mbele. Wenger aliendelea kudai kuwa ili kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao ni muhimu kubakiwa na nyota wake wote hivyo atajitahidi kuhakikisha hawaondoki.
No comments:
Post a Comment